Job 7:1-6

Ayubu: Mateso Yangu Hayana Mwisho


1 a“Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani?
Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa?

2 bKama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni,
au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake,

3 cndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili,
nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku.

4 dWakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’
Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko.

5 eMwili wangu umevikwa mabuu na uchafu,
ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha.

Ayubu Anamlilia Mungu


6 f“Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma,
nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini.
Copyright information for SwhKC